SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, July 14, 2010

Rais Kikwete afanywa mtemi Urambo!! Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete muda mfupi baada ya kuvikwa mavavi ya kijadi kama mtemi na malkia wa Wanyamwezi leo wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Urambo Mshariki leo mchana(picha na Freddy Maro)
Mke wa Rais Kikwete mama Salma Kikwete akivishwa joho kwa ajili ya kumsimika kama mlezi wa Mke wa Mtawala wa Kabila ya Wanyawezi. zoezi hilo lilifanyika mara baada ya Rais Kikwete kutawazwa leo wilayani Urambo kuwa kiongozi wa Kabila la Wanyamwezi.
(Picha na Tiganya Vincent)-MAELEZO-Urambo Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Aden Rage (kulia) akishirikiana na Spika wa Bunge la Tanzania Samwel Sitta kumsindikiza Rais Kikwete leo mjini Urambo mara baada ya uzinduzi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki.
Rais Kikwete afungua ofisi ya Mbunge Urambo Mashariki!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe na kufunua kitambaa kufungua rasmi ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki leo asubuhi.Pembeni ya Rais ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika Samuel Sita.
JK akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Aliyesimamam ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta.
JK akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge akiwakaribisha waheshimiwa wabunge mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege Urambo kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Kushoto ni Mbunge wa Mafia Mhe. Abdukarim Shah
JK akiwahutubia mamia ya wananchi wa Urambo mkoani Tabora wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Mbunge wa jimbo la Urambo Mshariki leo. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
(Picha na Freddy Maro)

0 comments:

Post a Comment