Mwanasayansi Muirani aliyetekwa nyara na Marekani aelekea nyumbani |
Mwanasayansi
Muirani Shahram Amiri ambaye alitekwa nyara na mashirika ya kijasusi ya
Marekani na Saudi Arabia mwaka jana ameondoka Marekani akielekea Tehran,
mji mkuu wa Iran. Msomi huyo Muirani alikimbilia hifadhi katika Kitengo cha Maslahi ya Iran katika Ubalozi wa Pakistan mjini Washington Jumanne na kuomba arejeshwe Iran mara moja. Ubalozi wa Pakistan unalinda maslahi ya Iran huko Marekani kwa sababu nchi hizi mbili hazina uhusiano wa kidiplomasia. Majasusi wa Marekani wakishirikiana na wenzao wa Saudia walimteka nyara Amiri alipokuwa katika ibada ya Umra nchini Saudi Arabia mwezi Juni 2009 na baada ya kutekwa nyara alipelekwa Marekani. Katika mikanda ya video aliyotoa, Amiri alisema alitekwa nyara na majasusi wa Marekani wakishirikiana na kikosi cha kijasusi cha Saudia kijulikanacho kama Istikhbarat mjini Madina. Wadadisi wa Mambo wanasema mashirika ya kijasusi ya Marekani yameamua kumuachilia huru Amiri baada ya kushindwa kumtumia katika propaganda zao dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran. Amiri amesema aliteswa sana alipokuwa mikononi mwa makachero wa Marekani. http://kiswahili.irib.ir
**********************
Mwili wa makamu wa rais wa chama cha upinzani nchini Rwanda
wapatikana
Mwili huo wa Andre Kagwa Rwisereka
umepatikana karibu na gari lake lililokuwa limetelekezwa.
Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Mwili wa Makamu wa Rais wa chama cha upinzani ambacho
hakijasajiliwa nchini Rwanda cha Democratic Green, Andre Kagwa
Rwisereka, hatimae umepatikana karibu na gari lake. Rwisereka
alikuwa hajulikani alipo baada ya gari lake kukutwa limetelekezwa
karibu na mji wa Butare. Haya yametokea wakati kukisalia wiki
chache kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo mwezi ujao.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi pamoja na chama cha
Democratic Green imethibitisha kupatikana kwa mwili wa Bwana
Rwisereka aliyetangazwa kutojulikana alipo mapema jana. Gari la
makamu huyo wa rais wa chama hicho cha upinzani lilikutwa karibu
na mto Mukula mjini Butare. Msemaji wa polisi Eric Kayiranga
amesema mwili wa Bwana Rwisereka umepatikana majira ya
asubuhi ya leo umbali wa kilometa tatu kutoka eneo ambako gari lake
lilionekana, huku kukiwa na kisu kikubwa kinachodhaniwa ndicho
kilitumika katika mauaji yake. Kayiranga amesema watu waliomuona
usiku kabla ya kutoweka wamesema alikuwa na fedha nyingi, hivyo
wanahisi huenda lilikuwa ni tukio la ujambazi na kwamba uchunguzi
wa tukio hilo tayari umeshaanza. Msemaji huyo wa polisi amesema
mwili huo umekutwa ukiwa na majeraha kifuani na umepelekwa
hospitali.
Bwana Habineza amesema chanzo cha mauaji hayo bado
hakijajulikana na kwamba sasa na yeye anaishi kwa woga kwa
sababu hapo awali alishawahi kupokea vitisho kutoka kwa watu
wasiojulikana. Chama cha Democratic Green kimekuwa kikishindwa
kupata usajili utakaokiwezesha kushiriki katika uchaguzi wa urais
uliopangwa kufanyika mwezi ujao. Kwa upande mwingine mashirika
ya kutetea haki za binaadamu yameilaumu serikali ya Rwanda kwa
kukandamiza wapinzani pamoja na vyombo vya habari kuelekea
kwenye uchaguzi huo. Aidha, Rwanda imekanusha tuhuma hizo
ikisema kuwa serikali imekuwa ikifanya mazungumzo na kukubaliana
na baadhi ya maoni ya wapinzani tangu yalipotokea mauaji ya
kimbari mwaka 1994.
Hata hivyo, polisi nchini Rwanda wamemkamata mwandishi habari
wa kujitegemea kwa tuhuma za kumfananisha Rais Paul Kagame na
kiongozi wa Manazi a Ujerumani, Adolf Hitler. Polisi imelithibitisha
hilo, ingawa afisa wa polisi amekanusha kuwa kukamatwa kwake
kunahusiana na uchaguzi mkuu ujao. Msemaji wa polisi nchini
Rwanda, Eric Kayiranga alisema kuwa Saidati Mukabibi, mwandishi
wa gazeti la kujitegemea la Umurabyo alikamatwa kwa kosa la
kukashifu, kuvuruga usalama wa nchi na ubaguzi wa kikabila. Baraza
la habari la Rwanda-MHC limesema kukamatwa kwa Mukabibi
hakuhusiani na uchaguzi ujao, ambao Rais Kagame anategemewa
kushinda kwa kupata wingi wa kura.
Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (RTRE)
|
0 comments:
Post a Comment