SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 28, 2011

MTANANGE LEO SIMBA YA TANZANIA V/S WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO.

Kikosi cha Simba. 
Kikosi cha Wydad Casablanca  cha Morocco.
Klabu ya Simba ya Tanzania leo inatarajiwa kuunguruma wakati itakapovaana na Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco katika mechi ya raundi ya tatu ya Ligi ya klabu Bingwa Afrika itakayochezwa katika uwanja wa Metrospot jijini Cairo nchini Misri.
Simba na Wydad zilipzta nafasi ya kucheza raundi ya tatu na mshindi kufuzu robo fainali ya ligi ya klabu bingwa kwenye uwanja huru baada ya Simba kushinda rufaa yao dhidi ya mchezaji Janvier Besala Bokungu wa TP Mazembe aliyechezeshwa na mabingwa hao wa zamani kinyume cha utaratibu.
Timu itakayofungwa leo itashiriki michuano mingine ya Kombe la Shirikisho.
Naitakia Simba kila la kheri iweze kushinda mechi ya leo na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo na kuiletea sifa Tanzania kwa ujumla.
Mungu Ibariki Simba Sports Club.
Mungu ibariki Tanzania.

0 comments:

Post a Comment