SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 15, 2014

PICHA NA TAARIFA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA: WATUMISHI OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA WAPIGWA MSASA JUU YA ELIMU YA UKIMWI MAHALA PA KAZI

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akifungua mafunzo ya Ukimwi mahali pa kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mwishoni mwa juma, Semina hiyo iliyoandaliwa na idara ya maendeleo ya jamii na mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa kwa watumishi hao ilikua na lengo la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayohusu janga la Ukimwi na umuhimu wa Tohara kwa wanaume katika kujikinga na janga hilo. Katika hotuba yake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa hakusita kuonyesha hisia zake kali kwa watumishi watakaohusika katika rushwa za ngono na kusema kuwa watachukuliwa hatua kali bila ya utetezi wowote kutoka kwake.
Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa Ndugu Daniel Mwaiteleke akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu gonjwa la UKIMWI kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga.
Muwezeshaji wa mada ya magonjwa ya zinaa STD na STI Dkt. Lunyelele akiwasilisha mada yake kwa umahiri mkubwa bila ya kutafunatafuna maneno
Dkt. Lunyelele akiwa anatoa mafunzo hayo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo.
Mjumbe katika Semina hiyo Ndugu Frank Mateny akichangia moja ya mada katika mafunzo hayo. 
Mdau Mussa Mwangoka na Paul Ngany'anyuka ndani ya Semina hiyo.
Dena na Richard Ndambala nao walikuwepo.Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com