SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 28, 2011

MKE WA WAZIRI MKUU WA INDIA MAMA GURSHARAN KAUR AISAIDIA WAMA MILIONI 15!!

Mke wa waziri Mkuu wa India Mama Gursharan Kaur(Kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi  milioni 15 mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) fedha ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo. Msaada huo umetolewa leo katika ofisi za WAMA zilizopo jijini 
Dar es Salaam.
 
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.
Na Anna Nkinda – Maelezo
Mke wa waziri Mkuu wa India Mama Gursharan Kaur ametoa msaada wa shilingi  milioni 15 kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleoo (WAMA) fedha ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo.
Msaada huo umetolewa leo katika ofisi za WAMA zilizopo jijini Dar es Salaam wakati mama Kaur alipoitembelea taasisi hiyo inayoongozwa na  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kufahamu  shughuli zinazofanywa na WAMA.
Akikabidhi  msaada huo Mama Kaur alisema kuwa ameguswa na kazi zinazofanywa na WAMA za kuisaidia jamii ya kitanzania, hivyo msaada huo utasaidia kutekeleza majukumu mbalimbali wanayoyafanya.
Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo yanayoikabili jamii ya kitanzania.
Alisema kuwa taasisi ya WAMA imekuwa ikipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo wa ndani na wa nje ya nchi hivyo aliwaomba wananchi wenye moyo wa kusaidia wasisite kufanya hivyo bila ya kuangalia kama msaada watakaoutoa ni mdogo au mkubwa.
Mama Kikwete alisema kuwa Taasisi ya WAMA imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa inawasaidia wanawake kuinua maisha yao, kuisaidia jamii ya watanzania kuwa na afya bora, kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa vijana na kada tofauti, kushughulikia uzazi salama  na kuwawezesha watoto wa kike ambao ni yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu.
Mama Kaur ameambatana na mumewe waziri Mkuu wa India Dr. Manmohan Singh aliyeko nchini katika ziara ya kikazi ya siku tatu.

0 comments:

Post a Comment