MWANAFUNZI KIPOFU ANAYEONGOZWA NA FARASI BADALA YA MBWA
Mona Ramouni akiwa na Cali.
MWANAMKE mmoja kipofu ametumia akiba ya fedha zake kununua farasi mdogo ili amsaidie kutembea sehemu anazotaka.
Wazazi wa Mona Ramouni hawakumruhusu kumleta mbwa katika nyumba ya familia yao kwani mnyama huyo huchukuliwa kama mchafu.
Hivyo, badala yake, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 alidunduliza fedha kwa muda wa miaka mitatu na kumnunua Cali, ambaye ni farasi mdogo mwenye urefu wa Sentineta 76 na amepewa mafunzo ya kumsaidia hata kutoka katika magari, kumwongoza katika makundi ya watu na sehemu zingine za ndani.
Ramouni (kushoto) akiwa darasani na farasi wake mdogo.
Mwanamke huyo ambaye anasomea mambo ya saikolojia alimpata farasi huyo kwa kupitia tovuti mnamo Aprili 2008 na anadai kwamba tangu amkaribishe Cali nyumbani kwake huko Dearborn, Michigan, Marekani, maisha yake yamebadilika sana.
"Ni farasi mzuri mdogo wa kike. Kitu ambacho ningekipenda ni kuwa na uwezo wa kumpeleka na yeye sehemu ambazo wote hatujazifika," anasema Ramouni na kuongeza: "Kabla ya kuwa na Cali nilikuwa nimekata tamaa lakini hivi sasa imani yangu niliyokuwa nayo utotoni, imerejea."
Ramouni alipoteza uwezo wake wa kuona baada ya kuzaliwa akiwa njiti miezi mitatu kabla. Hivi sasa, mwanamke huyo ambaye ni msomaji-mhakiki wa vitabu vya vipofu, ni mmoja wa watu watano tu nchini Marekani ambaye anatumia farasi kama mwongozaji wao
Chanzo: globalpublishers.info
Chanzo: globalpublishers.info
0 comments:
Post a Comment