SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, September 23, 2010

Timu ya soka ya Zob Ahan ya Iran yatinga nusu fainali ya klabu bingwa barani Asia

Sample Image
Timu ya soka ya Zob Ahan ya Iran imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la soka klabu bingwa barani Asia baada ya kuwalazimisha mabingwa watetezi timu ya soka ya Pohang Steelers ya Korea Kusini kutoka nayo sare ya bao moja kwa moja. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Isfahan Iran, Zob Ahan iliitandika timu hiyo ya Korea Kusini mabao mawili kwa moja. Katika mechi ya leo iliyokuwa ya vuta nikuvute, wenyeji Pohang Steelers wakishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao, walianza mchezo huo kwa kasi kubwa na kufanikiwa kujipatia bao katika dakika ya 10 tu ya mchezo. Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa bao hilo moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Zob Ahan ikijaribu kujipapatua ili kurejesha bao hilo, ilhali wenyeji timu ya soka ya Pohang Steelers wakijaribu kulinda bao lao. Katika dakika ya 80 ya mchezo mchezai machari wa Zob Ahan Muhammad Ridha Khalaatbari alifanikiwa kuzitikisa nyavu za Pohang Steelers na kuhuisha matumaini ya timu yake kusonga mbele. Kwa ushindi huo Zob Ahan imeingia nusu fainali na inatarajiwa kukutana katika mtanange huo na timu baina ya al-Hilal ya Saudi Arabia au al-Gharafah ya Qatar.

0 comments:

Post a Comment