Tume Huru ya Uchaguzi nchini Guinea CENI imependekeza Oktoba 10 kuwa tarehe ya kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi wa rais. Pendekezo hilo limekuja siku chache tu baada ya tarehe iliyokuwa imepangiwa uchaguzi huo Septemba 19 kuakhirishwa, kutokana na kukithiri kwa hali ya machafuko nchini humo. Naibu Mkuu wa CENI Hadja Aminata Mame Camara amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya mazungumzo ya kina yaliyovihusisha vyama husika. Hata hivyo, tarehe hiyo iliyopendekezwa lazima iidhinishwe na rais wa serikali ya mpito ya nchi hiyo Jenerali Sekouba Konate, ambaye anatarajiwa kurejea nchini humo leo hii akitokea nchini Mali, alikokuwa anahudhuria shrerehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa mkoloni Mfaransa. Wagombea Cellou Dalein Diallo waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo aliyepata asilimia 43 huku mwanasiasa mkongwe Alpha Conde aliyepata asilimia 18 katika uchaguzi wa duru ya kwanza uliogubikwa na utata, ndio watakaochuana katika kinyang'anyiro hicho.
Thursday, September 23, 2010
Guinea yapendekeza tarehe ya kufanyika uchaguzi wa duru ya pili
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, September 23, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment