SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, September 23, 2010

Morgan Tsvangirai: Vikosi vya Polisi na Jeshi vyadumaza marekebisho


Sample Image
Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amevituhumu vikosi vya jeshi na polisi ya nchi hiyo kuwa vizingiti vikuu katika njia ya marekebisho ya katiba mpya ya nchi hiyo. Matamshi ya Tsvangirai yamekuja katika hali ambayo, serikali ya nchi hiyo imekuwa ikifanya mikutano tangu mwezi Julai, ili kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Mpambe wa Tsvangirai ameuawa huku wengine zaidi ya 5 wakijeruhiwa kwenye machafuko yaliyozuka nchini humo tangu siku ya Jumamosi kati ya makundi hasimu ya kisiasa, askari jeshi na askari polisi ya nchi hiyo. 
Kwa mujibu wa makubaliano yaliyotiwa saini mapema mwaka jana yaliyopelekea kubuniwa serikali ya mseto kati ya chama cha Rais Robert Mugabe na cha Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai kufuatia uchaguzi wa 2008 uliogubikwa na utata, pande hasimu zilikubaliana na udharura wa kupatikana katiba mpya kabla ya uchaguzi mwingine mkuu kufanyika nchini. 

0 comments:

Post a Comment