SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, September 23, 2010

Ahmadinejad: Netanyahu ni katili anayefaa kupandishwa kizimbani

Sample Image
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtaja waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel kuwa katili mkubwa ambaye anastahili kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria vya kimataifa kutokana na jinai alizofanya dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina. Akizungumza katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Marekani CNN, Rais Ahmadinejad amesema Netanyahu anafaa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya mauaji ya wananchi madhulumu wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawalahuo na pia kuhusu uzio wa kibaguzi katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Rais wa Iran ya Kiislamu amevikosoa vyombo vya habari vya Marekani kwa kutowajibika na kutoueleza ulimwengu ukweli kuhusu Netanyahu na utawala ghasibu wa Israel. Amekumbusha kuwa silaha za nyuklia za Marekani na Israel ndilo tishio kuu kwa usalama wa ulimwengu tawala mbili za kibeberu ambazo amesema zimekuwa zikishirikiana kuishinikiza Iran, ili kufunika jinai zao. Ahmadinejad amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima itakuwa katika mstari wa mbele kupiga vita umiliki wa silaha hatari za nyuklia. 

0 comments:

Post a Comment