Teresa Lewis mwanamke mwenye umri wa miaka 41 mwenye matatizo ya akili amenyongwa leo nchini Marekani kwenye jimbo la Virginia, kwa kosa la kumuua mumewe na mjukuu wake wa Kambo.
Teresa ni mwanamke wa kwanza kuhukumiwa adhabu ya kifo nchini Marekani tangu mwaka 1912 na amesubiri kutekelezewa adhabu hiyo kwa muda wa miaka mitano.
Mwanamke huyo ameuawa kwa kudungwa sindano ya sumu. Maswali mengi yamejitokeza kuhusiana na uwezekano wa mama huyo aliyekuwa na kiwango cha akili cha IQ 72 kupanga na kutekeleza mauaji hayo ya watu wawili, ambaye pia imejulikana alikuwa na matatizo ya akili.
Mahakama kuu ya Marekani na Gavana wa jimbo la Virginia walikataa kuondoa adhabu hiyo ingawa wengi wametilia shaka kesi hiyo na maelfu ya watu walitaka iondolewe. Virginia ni jimbo la pili nchini Marekani linaloongoza katika utendaji vitendo vya jinai.
0 comments:
Post a Comment