Mwana wa kiume wa Gaddafi aikosoa vikali serikali ya baba yake
Mwana wa kiume wa kiongozi wa Libya Saiful Islam Gaddafi ameikosoa vikali serikali ya nchi hiyo akisema kuwa haina uwezo wa kuendesha nchi. Saiful Islam ambaye anatazamwa kama mrithi wa Kanali Gaddafi katika uongozi wa Libya ameishambulia serikali ya nchi hiyo baada ya kutembelea chumba cha nchi hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Shanghai huko Uchina. Amesema serikali ya Tripoli haikuchukua hatua za maana za kushughulikia chumba cha Libya katika maonyesho hayo ya kimataifa akisema hakuna serikali nchini Libya.
Matamshi hayo ya Saiful Islam Gaddafi yanaakisi migawanyiko inayotawala safu za watawala wa Libya na ushindani mkubwa wa kuwania madaraka uliopo kati ya kambi ya mwanasiasa huyo kijana inayotaka marekebisho na ile ya wazee na wasaidizi wa baba yake.
Wachambuzi wanasema Saiful Islam ndiye nayeonekana kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuongoza Libya baada ya baba yake Muammar Gaddafi lakini atalazimika kwanza kuwabwaga wahafidhina katika serikali, jeshi la Libya na vyombo vya upelelezi vya nchi hiyo.

0 comments:
Post a Comment