Manouchehr Muttaki Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, nchi za Magharibi zitajuta. Akizungumzia vikwazo vya upande mmoja visivyokuwa vya kiadilifu vya Marekani na Umoja wa Ulaya dhidi ya wananchi wa Iran, Muttaki amesisitiza kuwa, nchi za Magharibi zitakuja kujuta kutokana na nyendo zao zisizokuwa za kisheria na kimantiki kama ilivyotokea miaka iliyopita. Amesema kuwa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Umoja wa Ulaya ulichukua misimamo kama hiyo ya kijuba dhidi ya Iran, na kupelekea Tehran kuimarisha mashirikiano yake na nchi za maeneo mengine. Akizungumzia vitisho vinavyotolewa mara kwa mara na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Manouchehr Muttaki amesema kuwa, utawala wa Israel na Marekani zinaelewa wazi kwamba, kama zitaanzisha vita dhidi ya Iran, basi nhci hizo hazitakuwa na uwezo wa aina yoyote wa kusimamisha vita hivyo.
Thursday, August 12, 2010
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran: Nchi za Magharibi zitajuta
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, August 12, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment