Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia wametoa mkono wa pongezi kwa wananchi wa nchi zao na Waislamu wote duniani kwa mnasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wakizungumza kwa njia ya simu viongozi hao pia wametoa wito kwa ulimwengu wa Kiislamu kuzidisha udugu na mshikamano hususan katika mwezi huu wa toba na baraka. Rais Ahmadinejad amewaomba Waislamu kote duniani kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu kwa kukithirisha ibada. Kwa upande wake Mfalme Abdullah amesema huu ni mwezi wa mavuno ya thawabu na kwa mantiki hiyo Waislamu wanapaswa kutumia fursa hiyo barabara. Inafaa kukumbusha hapa kuwa ibada ya Saumu ni nguzo ya nne ya Uislamu na kila Muislamu analazimika kutekeleza ibada hiyo isipokuwa wale walio na sababu zinazokubalika kisheria.
Thursday, August 12, 2010
Ahmadinejad na Abdullah wawapongeza Waislamu kwa kuanza mfungo wa Ramadhani
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, August 12, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment