Meles Zenawi Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa, nchi yake iko tayari kwa mara nyingine tena kuwarejesha nchini Somalia, askari wa kulinda amani kwa shabaha ya kulinda amani na uthabiti nchini Somalia chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika. Zenawi ameongeza kuwa, vikosi vya Ethiopia vinaweza kuingia nchini Somalia, pindi tu vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika vilivyoko mjini Mogadishu vitakuwa hatarini. Amesema kuwa, majeshi ya Ethiopia yako tayari kuvisaidia kikosi cha askari elfu sita cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, iwapo viongozi wa Umoja wa Afrika watataka jeshi la Ethiopia lipelekwe nchini Somalia. Kuanzia mwaka 2007 hadi sasa, ni nchi mbili tu za Uganda na Burundi ndizo zilizopeleka askari wake wa kulinda amani nchini Somalia kwa shabaha ya kukabiliana na makundi ya waasi wa al Shabaab na Hizbu Islam ambayo yanatishia kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia.
Thursday, August 12, 2010
Zenawi asema Ethiopia iko tayari kupeleka askari wa kulinda amani Somalia

Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, August 12, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment