SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, August 19, 2010

WAGOMBEA URAIS WA CHADEMA NA NCCRA NAO WAREJESHA FOMU!!

Wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa kushoto na Mgombea Mwenza Khamis Hamad Khamis mara baada ya kurejesha fomu zao katika ofisi za tume hiyo leo jijini Dar es salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipanga kuwa Wagombea wote wanatakiwa kuwa wamerudisha fomu leo Agost 19 na kesho Agosti 20 ndiyo kampeni zinaanza rasmi kwa vyama vyote ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Wanachama wa Chama CHADEMA wakishangilia nje ya ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa wakati walipomsindikiza wagombea wa urais kupitia chama hicho wakati waliporejesha fomu katika Tume hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia akiwa katika msafara nawanachama wa chama hicho katika maeneo ya Moroco Konondoni jijini Dar es salaam mara baada ya mgombea wao kurudisha fomu leo hii katika tume ya ya Taifa ya Uchaguzi.
Wanachama wa chama cha NCCR Mageuzi wakiwa katika msafara katika maeneo ya Moroco Kinondoni mara baada ya mgombea wao kurejesho fomu za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.

0 comments:

Post a Comment