MAHOJIANO NA ISSA MICHUZI JUU YA UJIO WA MICHUZIPOST.COM
Upende,usipende,leo
hii unapoongelea masuala ya nyanja ya habari na mawasiliano kupitia
zana za blog kwa upande wa Tanzania(Tanzanian Blogsphere), huwezi
kuepuka kumtaja Muhidin Issa Michuzi a.k.a Ankal,Mzee wa Libeneke.
Mwanzoni
alipoanzisha blog yake maudhui yake yalikuwa zaidi ni picha na maelezo
kidogo juu ya picha hiyo au picha hizo.Hiyo ilitokana na ukweli kwamba
Michuzi ni seasoned professional photographer.
Baada ya muda
fulani,na kutokana na mafanikio aliyokuwa ameyapata,ilimlazimu kutanua
wigo wa blog yake na hivyo kutoishia katika picha na maelezo mafupi
mafupi tu bali kujumuisha maelezo au habari zaidi.Leo hii,blog yake
imekuwa kimbilio la wengi pale wanapotafuta habari motomoto kuhusu
kinachoendelea nchini Tanzania,maeneo ya jirani na hata sehemu
mbalimbali za ulimwengu.
Hivi sasa yupo
mbioni(keshazianza mbio zenyewe) kuboresha zaidi kazi ngumu anayoifanya
ya kuendeleza “libeneke”.Ameanzisha tovuti/blog mpya inayopatikana
kupitia http://michuzipost.com
BC imepata
nafasi ya kuongea naye machache kuhusu ujio huo wa MichuziPost na mambo
mengine kuhusiana na tasnia ya habari na mawasiliano. Je,”wadau”
watarajie nini katika uwanja huo mpya?Nini siri ya mafanikio yake mpaka
hivi sasa?Ana ushauri gani kwa bloggers wapya na wale wanaofikiria
kuanzisha blog?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Kwanza nikupe Hongera nyingi kwa kazi nzito unayoifanya.Mambo yanakwendaje?
MICHUZI:
Ahsante sana, mambo mswano tu. Libeneke kwa kwenda mbele. Yaani baada
ya miaka mitano ya tufanikio kiduchu tulikopatikana, sasa ni wakati
muafaka wa kupiga hatua tano mbele, na kusaidia ujenzi wa taifa letu
kwa njia ya habari.
Nitakuwa mtovu wa hisani na fadhila endapo kama nitaanza kujieleza
bila kwanza kuwashukuru wadau wa Globu ya Jamii popote walipo duniani,
kwani bila sapoti yao sidhani kama ningefikia robo tu ya hapa nilipo.
Naomba kwa
heshima na taadhima wape AHSANTE SANA wadau. Waambie nawapenda,
nawaheshimu na nitandelea kuwa mtumishi wao wakati wa raha na wakati wa
shida. Pia naomba ninaowaudhi kwa njia moja ama nyingine wanisamehe
kwani mie ni binadamu na si kamilifu. Pia si rahisi kumridhisha kila
mdau kwa kila jambo. Napenda sana kutumia ule msemo wa ‘what’s good for
the goose, is bad for the hen’. Hivyo naomba uvumilivu na kuelekezana
pale palipo na dosari.
habari zaidi bofya hapa: http://bongocelebrity.com/
0 comments:
Post a Comment