SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, August 19, 2010

WAGOMBEA WA URAIS CUF NAO WAREJESHA FOMU ZAO
Wagombea Urais kupitia Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba kushoto na Mgombea mwenza Duni Haji Duni wakipunga mikono yao mara baada ya kurejesha fomu zao katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dar es salaam leo ambapo wagombea kutoka vyama vyote vyote wanatarajia kuanza kampeni kesho nchini kote.
Viongozi wa Chama Wanachi CUF wakinyanyua juu mikono yao kuwapungia wanachama wa Chama hicho waliowasindikiza wagombea wao wakati waliporejesha fomu leo jijini Dar es salaam.
Wanachama wa chama cha CUF wakishangilia katika ofisi za Tume ya Uchaguzi leo wakati wagombea urais wa chama chao waliporejesha fomu Tume ya Uchaguzi leo.

0 comments:

Post a Comment