Wafanyakazi wa sekta ya umma Afrika kusini wakaidi amri ya mahakama
Wafanyakazi
wa sekta ya umma nchini Afrika Kusini wamekaidi amri ya mahakama ya
kuwataka wasitishe mgomo na kurudi kazini mara moja na badala yake
wameendeleza mgomo wao ambao umeingia siku ya saba hii leo. Polisi
wamelazimika kufyatua risasi za mipira ili kuwatawanya waandamanaji
waliokuwa wakiziba barabara na hospitali mjini Johannesburg. Imeripotiwa
kuwa takriban waandamanaji 60 wametiwa nguvuni na huenda wakapandishwa
kizimbani kwa kuzusha fujo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.
Jumamosi iliyopita serikali ya Afrika Kusini ilifanikiwa kupata kibali cha mahakama kinachopiga marufu mgomo huo ambapo Wizara ya Huduma za Jamii ilipewa idhini ya kuwaachisha kazi wafanyakazi watakaokataa kurudi kazini.

0 comments:
Post a Comment