Ajali ya ndege yaua watu 42 nchini China
Watu
wasiopungua 42 wamefariki dunia baada ya ndege ya shirika moja la ndege
la China kuanguka wakati ilipokuwa ikijaribu kutua katika hali mbaya ya
hewa ya ukungu mzito, katika ajali kubwa zaidi ya anga kutokea nchini
humo kwenye kipindi cha miaka sita iliyopita. Watu 54 wamenusurika
katika ajali hiyo iliyopelekea ndege ya shirika la ndege la Henan
iliyokuwa na abiria 96 kupasuka vipande vipande. Ajali hiyo imetokea
kaskazini mashariki mwa mji wa Yichun ulioko kwenye jimbo la
Heilongjiang. Kwa mujibu wa shirika la habari la China Xinhua, rubani wa
ndege hiyo ni miongoni mwa manusura wa ajali hiyo, hata hivyo
ameshindwa kuzungumza chochote hadi sasa kutokana na majeraha makubwa
aliyopata usoni. Huku timu ya waokoaji ikiendelea kupekua mabaki ya
ndege hiyo, majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali nne
za mji huo wa Yichun. Hadi sasa chanzo hasa cha ajali hiyo bado
hakijajulikana..
0 comments:
Post a Comment