Ban Ki-Moon akasirishwa na ubakaji wa wanawake uliofanywa na waasi wa Kihutu DRC
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kukasirishwa mno na
ubakaji wa wanawake uliofanywa na waasi wa Kihutu huko mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuamua kutuma mjumbe maalumu
kufuatilia kadhia hiyo. Kwa mujibu wa msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Martin Nesirky, kwa uchache raia 154 wa Congo walibakwa wakati
wa shambulio lililofanywa na waasi wa Kihutu wa Rwanda. Hata hivyo kwa
mujibu wa maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa wanawake 179 wamenajisiwa
katika kipindi cha majuma ya hivi karibuni. Nesirky amevielezea vitendo
hivyo kuwa mfano mwingine wa ngono za utumiaji nguvu na ukosefu wa
usalama unaotawala nchini Congo. Ameongeza kuwa kutokana na uzito wa
suala hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameamua kumtuma huko nchini
Congo Atul Khare ambaye ni Naibu wake anayeshughulikia Operesheni za
Kusimamia Amani.
0 comments:
Post a Comment