SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, August 16, 2010

Liverpool, Arsenal ngoma droo

LONDON, England

PAMOJA na kucheza pungufu zaidi ya dakika 45 za kipindi cha pili, timu ya Liverpool jana, ilifanikiwa kuibana Arsenal na kutoka nayo sare ya bao 1-1 kwenye mchezo mkali uliopigwa kwenye Uwanja wa Anfield.

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili na wa kwanza kwa kocha mpya wa Liverpool, Roy Hudgson aliyejiunga na timu hiyo akitokea Fulham.
Liverpool walipata pigo mapema kipindi cha kwanza baada ya winga wao Joe Cole kupewa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu mbaya beki wa Arsenal Laurent Kosciely ambaye naye alipewa kadi ya pili ya njano dakika tisini ya mchezo baada ya kuunawa mpira uliopigwa na Fernando Torres.
Katika mchezo huo, Liverpool ndiyo walikuwa wa kwanza kujipatia bao lao kupitia kwa David Ngog, ambaye alimalizia pasi safi toka kwa kiungo Javier Mascherano katika dakika ya 47 ya mchezo.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kushambuliana kwa zamu, Arsenal ilijipatia bao la kusawazisha kupitia kwa Mourine Chamakh ambaye alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Thomas Rosicky ambaye alipiga krosi safi langoni mwa Liverpool. 

0 comments:

Post a Comment