Wagombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, kushoto Rais Jakaya Kikwete
na Mgombea Mwenza Mohamed Ghalib Bilal wakionyesha fomu zao kwa
wanachama wa CCM waliowasindikiza wakati walipochukua fomu za kugombea
urais kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa leo asubuhi, wagombea
hao wanatarajia kurudisha fomu hizo kwenye tume ya uchaguzi Agosti 19
mwaka huu mara baada ya kukamilisha taratibu za kuzijaza, anayepiga
makofi ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Pius Msekwa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha
Mapinduzi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea fomu za kugombea urais
kutoka kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame leo katika
ofisi za Tume hiyo jijini Dar es salaam, Wagombea hao wanatakiwa
kurejesha fomu hizo Agosti 19 mwaka huu katika ofisi za tume ya
Uchaguzi.
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete (kulia)na Mgombea Mwenza Mh. Mohamed
Ghalib Bilal wakisaini fomu zao mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti
wa Tume hiyo Jaji Lewis Makame hayupo pichani katika ofisi za Tume ya
Uchaguzi leo hii.
Akina mama na watoto wakishangilia huku wakiwa wameshika bendera za
Chama Cha Mapinduzi wakati wana CCM mbalimbali walipomsindikiza Mgombea
wa urai kupitia chama hicho Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea
Mwenza wake Mh. Mohamed Ghalib Bilal walipochukua fomu zao katika ofisi
za Tume ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment