Agathon Rwasa aondolewa kinara wa FNL
Mzozo
a kisiasa unaendelea kutokota nchini Burundi huku taarifa za hivi punde
zikiarifu kuwa kiongozi wa FNL Agathon Rwasaa ameondolewa mamlakani.
Kundi
moja la chama hicho limefanya kikao maalum ambapo Emmanuel Mibiro
aliyekihama FNL na kujiunga na serikali aliteuliwa kiongozi . Mibiro
kwa sasa anahudumu kama mshauri wa Rais Nkurunziza. Jacques Bigirimana
ameteuliwa katibu Mkuu.
Hata
hivyo washirika wa Rwasa wamepuzilia mkutano huo na kuutaja kama njama
za serikali kukisambaratisha chama cha FNL. Makamu mwenyekiti,Alfred
Bagaya amesema Agathon Rwasa ndiye kinara wa chama cha FNL na kamba
hakuna kinara mwingine anayetambuliwa na wanachama.
Kundi
lililomtimua Rwasa limesema kuchukua hatua hiyo baada yake kutorokea
mafichoni na hivyo kuhujumu shughuli za chama hasa pale alipotangaza
chama hicho kususia uchaguzi mkuu Burundi.
Agathon Rwasa ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa rais Pierre Nkurunziza katika uchaguzi mkuu wa mwezi Juni.
Hata
hivyo aliongoza vyama vikuu vya upinzani kususia uchaguzi huo
akilalamikia dosari kwenye mfumo wa uchaguzi. Kwa sasa Rwasa yupo
mafichoni akihofia usalama wake.
Na kufuatia tukio la jana, kuna hofu ya kuzuka upya kwa vita.
0 comments:
Post a Comment