SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, March 27, 2011

TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS 2011

Hawa ndio ma-mc Milad Ayo na Penny katika Sherehe nzima za KILI MUSIC AWARDS 2011.
Pichani kulia ni mwanamuziki mkongwe kutoka bendi ya Msongo Ngoma Band,Mzee Mabella akionesha tuzo yake aliyoibuka nayo usiku wa kuamkia leo,tuzo hiyo ni imenyakuliwa na Mzee Mabella kuwa msanii binafsi ambaye hakuwahi kuhama bendi yako ya Msondo kwenda bendi nyingine tangu anaanza mziki (Tuzo binafsi ya Hall of Fame).
Waziri wa habari,vijana,utamaduni na michezo Dk.Emmanuel Nchimbi pichani Shoto akikabidhi tuzo ya taasisi,shirika la utangazaji la TBC kwa kuweza kuhifadhi nyimbo za wanamuziki kwa muda mrefu. (tuzo ya taasisi hall of Fame).
Mzee Yusuph akikabidhiwa tuzo yake ya wimbo bora wa taarabu uitwao Valentine kutoka Mchezaji wa mpira,Juma Kasseja.
Mapacha 3 nao waliibuka na tuzo yao wimbo bora wa kiswahili (bendi) uitwai Shika ushikapo.
Tuzo ya reppa bora ilinyakuliwa na mwanamuziki Khalid Chokoraa.
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House ,Khadija Mwanamboka akimkabidhi msanii wa kizazi kipya Linah tuzo ya msanii bora wa kike,Linah pia aliibuka na tuzo ya msanii mpya anayechipukia.
Tuzo ya wimbo bora wa hip hop ilinyakuwaliwa na msanii Joh Makini (kulia pichani) akiwa ameambatana na wasanii wenzake kadhaa.
Tuzo ya prodyuza bora ilikwenda kwa Lamar wa Fish Crub.
Msanii wa Bongo Flava,Ali Kiba akilishambulia jukwaa usiku huu ndani ya ukumbi wa diamond jubilee hall.
Msanii wa Bongo Flava,Diamond akiwaburudisha mashabiki usiku huu.
Wimbo Bora wa Reggae, What u Feel Inside - Hardmad.Msanii C-Pwaa alikabidhiwa tuzo yake ya video bora ya muziki wa mwaka uitwao ACTION aliomshirikisha DullySykes,Ngwair pamoja na Ms Trinity.C-Pwaa bia ameibuka na tuzo ya wimbo bora wa ragga/dancehall uitwa Action.
Wimbo bora wa RnB Nikikupata ulienda kwa msanii Ben Pol. Muigizaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya Mpoki tuzo yake ya wimbo bora wa asili wa Tanzania uitwao Shangazi.
Mwimbaji bora wa kike tuzo ilienda kwa Lady JD.
Pichani kushoto ni mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Combinations Sound a.k.a Combinenga,Man Water akipokea tuzo ya mwimbaji bora wa kiume (kwa niaba ya ) 20% kutoka kwa Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd Juhyana Kusaga,anaefuatia ni Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia TBL,David Minja.Katika hali ya shangwe furaha na vifijo vilivyotokea ukumbini,ambavyo vimesababishwa na msanii muziki wa kizazi kipya 20% ,kwamba ameweza kunyakua tuzo tano kuliko msanii mwingine yeyote aliyewahi kuchukua tuzo hizo tangu zianzishwe hapa nchini.
20% Akomba Tuzo za Kili Tanzania Music Awards 2011, Ukumbi Wazizima Kwa Shangwe ,haijawahi tokea!!

1.Tuzo ya wimbo bora wa Afro Pop-Tamaa mbaya.
2.Tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo.
3.Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume.
4.Tuzo ya wimbo bora wa mwaka.
5.Tuzo ya msanii bora wa muziki wa kiume.
Mdau Hot Pot akichukua tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki ambayo ilinyakuliwa na Kidumu pamoja na Lady jay dee.Lady Jay Dee pia alinyakuwa tuzo ya Mwimbaji bora wa kike.
Baadhi ya wasanii wa Hip Hop Kushoto ni msanii Bonta, JayMoe, K-singo, Nikki wa Pili na Ruben (Ncha Kali).
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Jay Moe na Jcb walinyakua tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana/kushirikishwa uitwao Ukisikia Paah!.

THT wakitumbuiza kwenye tuzo hizo.
Wahudhuriaji katika Tuzo za Kili Music Awards 2011 wakifuatilia kwa umakini.

0 comments:

Post a Comment