SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, August 1, 2010

WAZANZIBARI WALETA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
Na Juma Mohammed, Maelezo Zanzibar
Hatimaye wananchi waliopigakura ya maoni asilimia 66.4 wamekubali kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyoka Oktoba 31 mwaka huu. Matokeo hayo sasa yanaashiria kuzikwa kwa mfumo wa “Westminster” wa anayeshinda kuunda Serikali kwa kuchukua kila kitu, sasa kazi iliyobaki ni kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitisha mabadiliko ya Katiba Agosti 9 mwaka huu ili kuwepo kikatiba mfumo mpya wa muundo wa Serikali ya Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo leo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Khatib Mwinchande alisema waliochagua ndio wameshinda kwa kura 188,705 ikiwa ni sawa na asilimia 66.4 wakati waliochagua hapana wamepata kura 95,613 ikiwa sawa na asilimia 33.6.
Mwenyekiti huyo alisema idadi ya kura zote ni 293,339 sawa na asilimia 71 wakati waliojiandikisha ni 407,669 “Kwa matokeo hayo naomba kutangaza rasmin kwamba uchaguzi wa kura ya maoni iliyofanyika Julai 31 kura zilizosema ndiyo zimeshinda kwa asilimia 66.4” alisema Mwinchande huku wananchi waliohudhuria sherehe hiyo wakishangilia Kisiwani Pemba wananchi wengi wa huko wamechagua ndio wakati Mkoa wa ya Kusini Unguja kuna idadi kubwa ya watu waliochagua hapana.21,394 sawa na asilimia 66.3% waliochagua ndio 10,864 sawa na asilimia 33.7 katika Mkoa huo, kura zilizoharibika ni 934 ikiwa ni asilimia 2.8%. kura zote ni 33,192 ikiwa sawa na asilimia 69.1.
Mkoa wa Kaskazini Unguja wenye Majimbo manane ya Uchaguzi idadi ya kura za ndio ni 19,701(51%), kura za hapana ni 18,855(48%) zilizoharibika ni 1,730 sawa na asilimia 4.3 wakati kura zote ni 40,286 (65.1%). Kwa upande wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wenye Majimbo ya Uchaguzi 19, waliochangua ndio ni kura 69,406(61.4%) kura zote ni 115,811 ikiwa ni sawa na silimia 68.6 kura zilizoharibika ni 2,821.
Mkoa wa Kaskazini Pemba wenye Majimbo tisa kura za ndio ni 48,081(90.1%), zilizoharibika kura 1,764 sawa na asilimia 3.2 wakati kura zote ni 55,152 ikiwa ni sawa na asilimia 83.5. Mkoa wa Kusini Pemba wliochagua ndio ni 40,653(86.3%) wakati waliochagua hapana ni 6,473(13.7%) kura zote ni 48,598 swa na asilimia 77.3, zilizoharibika ni 1,472 sawa na asilimia 3.0.
Jumla ya kura 8,721 zimeharibika ikiwa sawa na asilimia 3 kwa Zanzibar nzima wakati kura halali zilikuwa 284,318 sawa na asilimia 97.0 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF) Seif Shariff Hamad alisema “Nimefurahishwa na matokeo ya kura ya maoni zilizopigwa na wananchi wa Zanzibar, ni matokeo yao yanayoonesha hisia za demokrasia”

0 comments:

Post a Comment