Ngeleja Amfagilia JK Kwa Kutekeleza Ahadi
alipotua Mwanza kuanza kampeni Kanda ya Ziwa
Mgombea pekee wa Ubunge jimbo la Sengerema wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini amemmwagia sifa kedekede Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa Sengerema kuomba kura kutetea kiti cha urais tiketi ya CCM.
Baadhi ya maeneo aliyoyataja Mh Ngeleja ni kama ifuatavyo:
1. Ujenzi wa barabara ya kwenda Geita, ambayo imekamilika kuanzia Wilaya hii ya Sengerema. Ujenzi wa kuunganisha barabara nyingine kama ile ya kwenda Buchosa kwa kiwango cha lami inaendelea. Barabara nyingine zilizokamilika ni ile ya Misungwi.
1. Ujenzi wa barabara ya kwenda Geita, ambayo imekamilika kuanzia Wilaya hii ya Sengerema. Ujenzi wa kuunganisha barabara nyingine kama ile ya kwenda Buchosa kwa kiwango cha lami inaendelea. Barabara nyingine zilizokamilika ni ile ya Misungwi.
2. Juhudi za kuunganisha Mwanza na nchi jirani kupitia kiungo cha Busisi na Bukongo zimemalizika. Pia juhudi za kuunganisha maeneo mbalimbali ya Mwanza kuvuka ziwa nazo zimefanyika na sasa kuna kivuko cha MV Misungwi. Pia ukarabati wa Kivuko MV Sengerema umekamilishwa na sasa Sengerema ina vivuko viwili.
4. Barabara nne kuu za kuingia na kutoka Sengerema zimejengwa kwa kiwango cha lami na hivyo kurejesha usafiri wa mabasi yaliyopotea miaka 20 iliyopita sasa umerudi.
5. Kwenye upande wa elimu, 2005 Sengerema ilikuwa na shule sita tu na sasa kuna shule zaidi ya 21 za sekondari. Sekta ya elimu imepewa kipaumbele sana kwenye jimbo la sengerema kwa juhudi za Mheshimiwa Rais Kikwete.
6. Vituo vya afya vimejengwa na huduma ya afya imeimarika, yote hayo ilikuwa ni jitihada za Mheshimiwa Rais na Serikali ya Awamu ya Nne.
7. Mradi wa Umeme - Jimbo la Sengerema na lile la Buchosa tuko kwenye mpango wa MCC ambapo majimbo haya mawili yatawaka taa muda si mrefu. Utaratibu wa kumpata mkandarasi aliyeshinda tenda umeanza na ataanza kutekeleza mpango huu mkubwa muda si mrefu. Pia kwenye umeme tuna mradi mwingine unaofadhiliwa na serikali wa kuleta umeme vijijini REA.
8. Maji: Suala la maji limesumbua sana wakazi wa Sengerema, lakini viongozi wa Wilaya wameamua kusimamia fedha za utekelezaji wa mradi huu ili kuhakikisha tatizo hili litatuliwe.
Mwisho Mbunge wa Sengerema Mh. Ngereja amemshukuru Rais Kikwete kwa kumpa dhamana ya kuongoza Wizara ya Nishati na Madini kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Ameeleza wana Sengerema kwamba amewaamini sana wao ndio maana amempa yeye madaraka hayo makubwa na nyeti.
Wakazi wa Sengerema walimsindikiza Mbunge huyo kijana kwa nderemo na vifijo huku wakiahidi kumchagua Rais Kikwete na wabunge na madiwani wote wa CCM kwa asilimia mia mbili!
0 comments:
Post a Comment