SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, August 23, 2010


Rais Ahmadinejad: Iran iko tayari kukabiliana na vikwazo vya aina yoyote ile

Sample Image
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amesisitiza kuwa, Iran iko tayari kukabiliana na vikwazo vyovyote vile vitakavyowekwa na nchi za Magharibi. Akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati ya baraza la mawaziri na wabunge, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, kama ilivyokuwa miaka iliyopita, vikwazo vinavyowekwa dhidi ya Iran, vitabadilishwa na kuwa fursa nzuri ya kuimarisha uchumi na kujitosheleza katika kila sekta hapa nchini. Ameongeza kuwa, leo hii majukumu mengi yametekelezwa na serikali na bunge, amma pamoja na hayo yamesalia majukumu mengine mengi zaidi ya kutekelezwa. Kwenye mazungumzo hayo, naye Dakta Ali Larijani Spika wa Bunge la Iran ameeleza kuwa, kikao kati ya pande mbili ni muhimu katika kuchunguza siasa kuu za kiuchumi, kisiasa na kilimo na kusisitiza kuwa, kila moja kati ya maudhui hizo zinapaswa kujadiliwa kivyake.

0 comments:

Post a Comment