Somaliland yapata rais mpya
Kiongozi wa upinzani katika eneo
lililojitenga na Somalia , Somaliland,Ahmed Mohamed Silanyo ametangazwa
kuwa mshindi kama ilivyotegemwa na wengi katika uchaguzi mkuu wa urais
wa wiki iliyopita.
Uchaguzi wa Rais uliopita mjini Hargeisa aliposhinda Dahir
Riyaleh Kahin.
Somaliland ambayo ilaitawaliwa na Uingereza wakati ambapo sehemu
iliyobakia ya Somalia ilitawaliwa na Italia, ilijitangzia uhuru wake
mwaka
1991.Kwa upande mwengine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
ameitaka Somalia ambayo inaadhimisha miaka 50 ya uhuru wake,
kutafuta njia za kurejesha umoja.
Matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Somaliland yanaonesha
kuwa kiongozi huyo wa chama cha upinzani Tulmiye Unity amepata 49.59
asilimia ya kura zilizopigwa, wakati ambapo Rais Dahir Rayale Kahin
amepata
33.23 asilimia.Chama cha Haki na Jamii kilipata asilimia 17.18 na kukiri
kushindwa.
Uchaguzi mkuu
Kiasi ya watu millioni 1 na elfu 9 walijiandikisha kupiga kura
miongoni mwa
raia millioni tatu unusu wa eneo hilo, ambapo waliyoweza kupiga kura
walikuwa ni laki tano na elfu 38.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya
Somaliland Essa Yusuf Mohammed amesema uchaguzi huo ni muhimu kwa
wananchi wa wa eneo hilo na pia ni hatua moja kubwa kuelekea demokrasia
kamili.Rais huyo mteule wa Somaliland Ahmed Mohamed Silanyo, katika
uchaguzi uliyopita mwaka 2003, alishindwa na Rais Kahin ambaye alipata
asilimia 80 ya kura zote.Kwa mujibu wa katiba ya Somaliland, mahakama
kuu
inatakiwa kuthibitisha matokeo ndani ya kipindi cha siku 15 baada ya
kutangazwa.
Mji wa Hargeisa
Waangalizi wa kimataifa walisema kuwa uchaguzi huo, ulikuwa huru na
wa
haki, pamoja na kwamba kulikuwa na kasoro ndogo zilizojitokeza, kama
vile
chama tawala kutumia fedha za serikali pamoja na magari na vyombo vya
habari vya serikali katika kampeni.
Kumbukumbu ya 50
Somaliland ambayo bado haijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kuwa
nchi
inayojitawala, zaidi ya kutambuliwa na Yemen tu, inajiweka mbali na
Somalia
ambayo imeshuhudia miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametumia nafasi ya
kuadhimisha miaka 50 tokea kwa Somalia yote kujipatia uhuru wake, kabla
ya
Somaliland na Puntland kujitenga,kutoa wito kwa nchi hiyo kutafuta njia
za
kurejesha umoja.
Ban Ki-moon amepongeza ushapavu na ujasiri wa wananchi wa Somalia na
kuwathibitishia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia kukabiliana
na
kuzishinda changamoto kubwa walizonazo na kufikia ndoto ya kuwa na
maisha ya amani, utulivu na mustakhbali mzuri.Katika taarifa yake hiyo
amewataka wasomali wageuke nyuma na kuangalia zama ambazo wananchi
wa nchi hiyo miaka 50 iliyopita walishikamana kwa hari na fahari wakiwa
na
mategemeo ya kuwa taifa lao imara.
Mauaji kwenye maadhimisho
Serikali ya Rais Sharif Sheikh Ahmed inayoungwa mkono na mataifa ya
magharibi na ambayo inadhibiti maeneo machache katika mji mkuu
Mogadishu, inaadhimisha sherehe hizo za miaka 50 ya uhuru. Hata hivyo,
mamadhimisho hayo yalishuhudia watu 17 wakiuawa katika mapigano kati ya
majeshi ya serikali na wanamgambo wa kiislam.
Mapema Kundi la wanamgambo wa kiislam la Heb Al-Islam limewataka raia
kususia maadhimisho hayo na kuonya kuwashambulia wale watakaoshiriki.
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha mamtibabu ya dharura mjini Mogadishu,
Ali Muse, watu 11 wakiwemo watoto watano na wanawake watatu waliuawa
baada ya kombora kulipua jengo moja.Kituo cha radio kinachomilikiwa na
serikali kilitangaza kuwa Rais Sheikh Sharif Ahmed amekwenda mstari wa
mbele kwenye mapambano na wanamgambo hao wa kiislam.Picha za
televisheni zilimuonesha kiongozi huyo akiwa katika mavazi ya kijeshi
kwenye
eneo la mapambano.
Mwandishi:Aboubakary Liongo
0 comments:
Post a Comment