SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, July 2, 2010

Rais mpya wa Ujerumani apuuza madai
Rais mpya wa
 Ujerumani Christian Wulff
Rais mpya wa Ujerumani Christian Wulff
Rais mpya wa Ujerumani Christian Wulff amepuuza madai kuwa ushindi wake mwembamba ni pigo kwa serikali ya mseto ya mrengo wa kati kulia inayoongozwa na kansela Angela Merkel
Mwanasiasa huyo kutoka chama cha  Christian Democrat  alimshinda mgombea wa mrengo wa kati kushoto, Joachim Gauck katika uchaguzi wa urais hapo jana uliyochukua zaidi ya saa tisa na kulazimika kufanyika kwa duru tatu kabla ya mshindi kupatikana.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Ujerumani Bwana Wulff amesema ukweli kuwa mwishowe aliweza kupata wingi wa kura ni kitu kinachompa nguvu na hamasa.
Hata hivyo chama cha Christian Democratic kimekuwa kikitathmini tabia ya baadhi ya wabunge wake kutokuwa na nidhamu na chama. Christian Wulff alifanikiwa kupata ushindi huo dhidi ya Gauck, baada ya Kansela Angela Merkel na viongozi wenzake wa muungano wa vyama vinavyotawala kuomba kuwepo na mshikamano.
Kujiuzulu ghafla kwa Rais Horst Koehler lilikuwa  ni pigo jingine kwa serikali ya Kansela Merkel.
Wakati huo huo kiongozi  ndani ya bunge wa chama cha walinzi wa mazingira , Renate Künast, amesema kushindwa kwa  Joachim Gauck  kumehitimisha mapendekezo yoyote juu ya mustakhbali wa ushirikiano kati ya chama cha upinzani cha SPD chama chake na kile cha mrengo wa shoto, Die Linke.

Rais mpya wa Ujerumani kuapishwa leo  
Berlin:

Rais mteule wa Ujerumani, Christian Wulff, anaapishwa rasmi baadaye leo kuwa Rais mpya wa Ujerumani  katika kikao kitakachowajumuisha wabunge wa mabaraza yote mawili ya bunge la Ujerumani, Bundesrat na Bundestag.
Baada ya kuapishwa atatoa hotuba rasmi ya kwanza kama Rais.
Christian Wulff alichaguliwa Jumanne wiki hii baada ya zaidi ya saa tisa na duru tatu za upigaji kura bungeni, hali iliyoeleza kuwa ni aibu kwa Kansela Angela Merkel na muungano wake wa vyama vya mrengo wa kulia vya Christian Democrats, CDU/CSU, na Free Democrats, FDP, ambao sasa vinapaswa kukabiliana na tatizo la kutokuwa na umoja miongoni mwa wabunge wao.
Mpinzani mkubwa  wa Christan Wullf katika kuwania kiti hicho cha Rais alikuwa ni mgombea aliyepitishwa na upinzani, Joachim Gauck.
Mwandishi:Aboubakary Liongo

0 comments:

Post a Comment