Vita vya mtandaoni vyakaribia
Mkutano wa mizozo ya mtandaoni uliofanyika nchini Estonia
hivi karibuni .
Hadi hivi sasa kumefanyika vita vya ardhini, majini na
angani. Sasa kunakuja aina nyingine kabisa ya vita. Vita vya
mawasiliano mtandaoni. Hali inayozidi kukua ya kutegemea zaidi
miundo mbinu ya teknolojia ya mawasiliano inaelekeza katika
hali isiyo salama ya kushambuliwa mawasiliano hayo. Majeshi
pamoja na idara za usalama yamekwisha iona hali hiyo kwa muda
mrefu na wameanza kulishughulikia suala hilo kikamilifu.
Kwa kifupi, ufanisi wa kiuchumi wa Marekani katika karne ya
21, utategemea sana, usalama wa mawasiliano ya mtandao.
Ni ukweli usiokanika kutoka kwa rais wa Marekani Barack
Obama. Katika mwezi wa Mei , mwaka 2009 alikuwa rais wa kwanza
wa Marekani kuweza kuzungumzia katika hotuba yake kuhusu usalama
wa mawasiliano ya mtandao. Obama amesisitiza hatari ya
kutegemea mtandao wa kompyuta, mafuta na gesi, umeme na maji,
vitu ambavyo upatikanaji wake unaweza kuvurugwa pamoja na
usalama wa safari za ndege ulivyo katika hatari. Kutokana na
kukabiliwa na hali hii isiyo salama rais Obama anataka mfumo wa
kuulinda mtandao.
Ni kweli kwamba katika dunia ya leo vitendo vya ugaidi
vinaweza kutokea , sio tu kwa watu wachache wenye imani kali
wanaovaa mikanda ya kujilipua, lakini kwa kugusa vitufe vichache
tu katika kompyuta. Silaha ya amaangamizi.
Mwaka mmoja baada ya hotuba hii, tarehe 21 Mei 2010
Jenerali Keith Alexander alitunukiwa nyota yake ya nne. Mkuu wa
idara ya usalama wa ndani, NSA, na pia alipokea wadhifa wa
kamanda wa idara ya mawasiliano katika mtandao. Idara ya NSA
inakuwa idara kuu ya ujasusi na yenye mamlaka katika Marekani.
NSA ni mwajiri mkuu duniani hivi sasa wa wataalamu wa hesabu.
Kutokea katika makao yake makuu mjini Fort Mead, idara hii
inaangalia mawasiliano yote ya mtandaoni duniani kote, kuchunguza
na kutambua maandishi ya siri, pamoja na kuyatathmini. wakati
Keith Alexander alipoanza kazi rasmi kama mkuu wa kamandi ya
mawasiliano ya mtandaoni, hapo Juni 3, aliielezea hali kuwa ya
kutisha. Mara milioni sita kila siku, unashambuliwa mfumo wa
mtandao wa wizara ya ulinzi, anasema Alexander na hali hiyo
inaendelea.
Utajiri wa Marekani na nguvu zake unaifanya nchi hii kuwa
lengo la mashambulizi katika mtandao wa mawasiliano. Na moja
kati ya nguzo za nguvu zetu, jeshi letu, iko katika hatari,
huenda katika kiwango cha juu kabisa. Jeshi letu linategemea
mtandao wake ili kufanya udhibiti wa uongozi, mawasiliano, ujasusi,
uendeshaji na usafirishaji wa vitu mbali mbali. Katika idara ya
ulinzi tuna zaidi ya mashine milioni 7 za kuzilinda ambazo
zimeunganishwa katika karibu mitandao 15,000.
Mwaka mmoja uliopita waziri wa ulinzi wa Marekani Robert
Gates alisema kuwa idadi ya wataalamu wa usalama wa mtandao
wa kompyuta waongezwe mara nne. Na hii sio tu kwa ajili ya
kujilinda na kulinda mfumo wa nchi hiyo tu. Mtaalamu wa
masuala ya kompyuta nchini Marekani Herbert Lin , anazungumzia pia
kuhusiana baadhi ya mashambulizi haya. Anasema kuwa mataifa
kadha yanajaribu kujilinda na pia kushambulia katika mtandao.
Lakini mjadala wa wazi unatuwama hususan katika viwango vya
kujilinda. Ni watu wachache sana wameweza kuzungumzia kuhusu
viwango vya mashambulio, lakini hii ni sehemu muhimu ya sera
za usalama katika mtandao.
Mwandishi : Matthias von Hein / Sekione Kitojo.
0 comments:
Post a Comment