Hodgson kocha mpya wa Liverpool
Klabu ya Liverpool imemtangaza
Roy Hodgson kuwa meneja mpya wa klabu ya Liverpool baada ya kocha huyo
wa zamani wa klabu ya Fulham kutia saini mkataba wa miaka 3.
Hodgson anachukua nafasi ya Rafael Benitez
ambaye aliacha wadhifa huo kwa makubaliano na Liverpool, na sasa ni
meneja wa klabu ya Intermilan.
Msimu uliopita Hodgson aliiongoza klabu ya
Fulham hadi fainali ya Kombe la ligi ya Uropa, ambapo walipoteza kwa
Atletico Madrid.
Katika muda wa miaka 34 ambayo Hodgson amehudumu
kama meneja, Hodgson ameshazifundisha timu za taifa za Switzerland,
Muungano wa Imarati na Finland.
Intermilan ni miongoni mwa vilabu 12 ambavyo
Hodgson amevifundisha katika miaka hiyo.
Jukumu ambalo Mwingereza huyo atalipa umuhimu wa
kwanza katika Liverpool ni kuhakikisha anawadumisha katika Anfield
nahodha Steven Gerrard, mshambuliaji Fernando Torres na kiungo Javier
Mascherano.
Kumekuwa na mazungumzo ya uwezekano wa wachezaji
hao watatu kuondoka Liverpool kujiunga na vilabu vinavyoahidi pesa
nono.
Ni wachezaji ambao Liverpool itawahitaji sana
kufufua matumaini yao ya kurejea kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa
wa Ulaya baada ya kukosa nafasi ya kushiriki msimu unaokuja,
walipomaliza katika nafasi ya saba kwenye ligi ya primia ya England.
Mwenyekiti wa Liverpool Martin Broughton
amemhakikishia Hodgson kwamba hatahitaji kuuza wachezaji ili kuweza
kulipa deni kubwa la klabu hiyo linalofikia paundi milioni 350.
Hodgson alipigiwa kura ya kuwa meneja bora msimu
uliopita baada ya kuiongoza Fulham hadi fainali ya kombe la Ligi ya
Uropa, ambapo kabla ya hapo waliishinda Juventus ya Italia na Wolfsburg
ya Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment