Rais Ahmadinejad kuzitembelea Nigeria na Mali wiki ijayo
Rais Mahmoud
Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatazamiwa kuzitembelea nchi
za Kiafrika za Nigeria na Mali.Katika duru ya kwanza ya safari hiyo
wiki ijayo, Rais Ahmadinejad atafika Abuja, mji mkuu wa Nigeria kwa
lengo la kushiriki katika kongamano la D8 linalozileta pamoja nchi za
Kiislamu zinazoendelea.
Baada ya hapo anatazamiwa kuelekea Bamako mji mkuu wa Mali ambapo atafanya mazungumzo ya uhusiano wa pande mbili na wakuu wa nchi hiyo. Balozi wa Iran nchini Nigeria Khosro Rezazadeh amethibitisha kuwa rais Ahmadinejad ataitembelea nchi hiyo lakini hakutoa maelezo zaidi. Mwezi Aprili rais wa Iran alizitembelea nchi za Afrika za Uganda na Zimbabwe. Aidha mwezi Februari 2009 rais Ahmadinejad alizitembelea nchi za mashariki mwa Afrika za Kenya, Djibouti na Visiwa vya Comoro. Safari za mara kwa mara za Rais Ahmadinejad barani Afrika ni katika fremu ya sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kisiasa na nchi za Afrika.

0 comments:
Post a Comment