SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, July 2, 2010

Benki ya CRDB yaipiga jeki hospitali ya mkoa Dodoma

Waziri wa afya Mh. Prof. David Mwakyusa akiwasili katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa Dododma ili kupokea wodi na vifaa vilivivyotolewa na Benki ya CRDB, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Charles Kimei, Naibu Waziri wa Afya Mh.Dr. Aisha Kigoda na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.James Msekela. Waziri wa Afya Mh.David Mwakyusa akikata utepe kufungua rasmi wodi ya kinamama ya hospitali ya mkoa wa Dodoma iliyokarabatiwa kwa msaada wa Benki ya CRDB. Mh. Waziri akiongea na kinamama waliolazwa hospitali ya mkoa wa Dodoma iliyokarabatiwa kwa msaada wa Benki ya CRDB. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Kimei Waziri wa Afya Mh.David Mwakyusa, akifurahi vitanda vipya vilivyotolewa na Benki ya CRDB huku akishuhudiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei na Mkurugenzi wa Masoko Bi.Tully Mwambapa. Sehemu ya wodi ya hospitali ya mkoa wa Dodoma iliyokarabatiwa na CRDB

0 comments:

Post a Comment