SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 1, 2010

Rais Jonathan aifungia timu ya soka ya Nigeria kushiriki michezo kwa miaka 2

Sample ImageRais Goodluck Jonathan wa Nigeria ameifungia timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo kushiriki katika michuano ya aina yoyote kwa muda wa miaka miwili kutokana na matokea duni iliyodhihirisha katika mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Afrika Kusini. Mshauri Maalumu wa Rais Jonathan amewaambia waandishi wa habari kuwa, hatua hiyo itaiwezesha timu hiyo ya Nigeria kupanga upya mikakati ya kuimarisha mchezo wake kama hapo awali. Aidha, Shirikisho la Kandanda la Nigeria NFF litavunjwa na shirikisho la muda kubuniwa, na pia kupangwa jopo la kuchunguza tenda kazi za Kamati Andalizi ya Kombe la Dunia nchini humo. Timu hiyo maarufu kama Super Eagles ilibanduliwa katika michuano ya makundi bila kushinda hata mechi moja katika michuano ya Kombe la Dunia. 
******************************* 
Serikali ya Sudan yamwachia huru kiongozi wa upinzani Hassan Abdullah Turabi Sample Image
Serikali ya Sudan imemwachia huru kiongozi wa upinzani nchini humo Hassan al-Turabi baada ya kumfunga kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa kukosoa ushindi wa Rais Hassan al-Bashir katika uchaguzi uliopita. Turabi ambaye alitiwa kizuizini tangu Mei 16 mjini Khartoum siku chache baada ya uchaguzi uliomrudisha madarakani Rais al-Bashir, amedai mbele ya waandishi wa habari kuwa, polisi ilimshika bila ya sababu zozote za kimsingi. Turabi ameutaja utawala wa Rais al-Bashir kuwa ni wa kidikteta na kwamba polisi ilimkamata na kumwachilia bila ya kutoa kauli yoyote.
Maafisa usalama wa Sudan walimkamata kiongozi huyo wa upinzani nyumbani kwake jijini Khartoum kabla ya kuvamia kituo cha gazeti la chama chake na kuwazuilia wafanyakazi wake. Turabi ambaye alikuwa mpambe wa karibu wa Rais al-Bashir amekuwa akikamatwa mara kwa mara pale wanapozozana kisiasa na kiongozi huyo yapata miaka 10 sasa.

0 comments:

Post a Comment