KWA HERI MARCIO
MAXIMO
nAliyekuwa
kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo, ameagwa rasmi usiku wa
kuamkia leo katika hafla fupi iliyoandaliwa na TFF Msasani jirani na
shule ya Feza jijini Dar es salaam. Katika hafla hiyo, pamoja na mambo
mengine, Kocha Maximo alipewa zawadi mbalimbali ikiwemo ya kinyago
alichopewa na Mwenyekiti Mtendaji wa kiwanda cha Serengeti, Jaji Mark
Bomani.
Ni dhahiri kwamba kocha huyo atakumbukwa kwa kazi yake aliyoifanyia Tanzania japokuwa bado kuna wadau wa soka ambao wanasema hakufaya kitu ila tunaojua kusema asante tunasema Maximo amefanya kitu kikubwa katika soka letu lililokuwa la kichwa cha Mwendawazimu enzi hizo, na anastahili kupongezwa mpaka hapa alipotufikisha manake kuna methali inayosema "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni"
Yote kwa Yote tunasema Watanzania tunajifanya tunajua sana mpira wakati kujua kwetu kuko vinywani zaidi kuliko vitendo na kama ndiyo hivyo basi tukubali kwamba hatujui jamai.

kwa chanzo na picha na habari zaidi
0 comments:
Post a Comment