Mashirika
kadhaa ya kijamii yametoa taarifa ya kulaani hatua ya wabunge wa Kenya
ya kujiongezea mishahara huku nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikiendelea
kuzongwa na umasikini. Mkurugenzi wa shirika la Kenya Moja Bw. Mathew
Makori amesema kuwa kwa sasa Kenya inakabiliwa na wakati mgumu kiuchumi
na kwamba hatua hiyo ya wabunge imeonyesha ubinafsi wa viongozi hao.
Wabunge wa Kenya walipitisha kwa kauli moja muswada wa kuwaongeza mishahara siku ya Jumatano ambapo sasa mshahara wa mbunge utafikia shilingi milioni 1.2 kutoka shilingi laki nane unusu. Wananchi kwa upande wao wametishia kutoshiriki kwenye kura ya maoni ya Agosti 4 kuhusu katiba mpya iwapo rais Kibaki ataidhinisha sheria hiyo.
kiswahili.irib.ir

0 comments:
Post a Comment