Kwa akali watu 21 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, katika
mapigano makali yaliyotokea nchini Somalia. Taasisi ya Kutetea Haki za
Binadamu ya 'Ilman' yenye makao yake mjini Mogadishu imetangaza kuwa,
watu wasiopungua 14 wameuawa na wengine 24 kujeruhiwa kwenye mapigano
yaliyotokea kati ya makabila mawili kwenye kijiji kimoja kilichoko
katikati mwa nchi hiyo. Taasisi hiyo imeongeza kuwa, watu wengine saba
wameuawa na wengine kumi na nane kujeruhiwa, katika mapigano yaliyotokea
kati ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika na waasi wanaobeba
silaha wa kundi la ash Shabaab mjini Mogadishu. Taarifa ya taasisi ya
Ilman imeongeza kuwa, tokea mwaka 2007 hadi sasa, zaidi ya watu elfu
ishirini na moja wameuawa kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
nchini Somalia.
**********************
Mahakama ya ICTR yamfunga miaka 25 jela mshukiwa wa mauaji ya kimbari
**********************
Mahakama ya ICTR yamfunga miaka 25 jela mshukiwa wa mauaji ya kimbari
Mahakama ya
Kimataifa kwa ajili ya Rwanda ICTR imemhukumu kifungo cha miaka 25 jela
mshukiwa mkongwe wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda ambapo
kwa akali watu wasiopungua laki nane waliuawa wengi wao wakiwa wa
kabila la Watutsi. Yusuf Munyakazi mwenye umri wa miaka 75 amepatikana
na hatia ya kuhusika kwenye mauji hayo pamoja kuwabaka wanawake wa
Kitutsi waliokuwa wamekimbilia kwenye kanisa moja kutafuta hifadhi.
Munyakazi alitiwa mbaroni mwaka 2004 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo na kufikishwa kwenye mahakama hiyo yenye makao yake mjini Arusha
Tanzania.
kiswahili.irib.ir
kiswahili.irib.ir
0 comments:
Post a Comment