SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, July 14, 2010

Mamia waandamana Ufaransa kukosoa Ukoloni Mambo Leo Barani Afrika Sample Image
Mamia ya watu waliandamana jana mjini Paris wakiitaka Ufaransa kukomesha ukoloni mambo leo katika makoloni yake ya zamani barani Afrika. Waandamanaji hao wamelaani mwaliko uliotolewa na Rais Nicolas Sarkozy kwa viongozi wa nchi 13 za Kiafrika kwa ajili ya kushiriki kwenye sherehe za siku ya taifa ya Ufaransa zinazofanyika hii leo.
Waandamanaji hao wamesema lengo la mwaliko huo ni kutilia mkazo utiifu wa makoloni ya zamani ya Ufaransa kwa serikali ya Paris. Waandamanaji hao pia wamelaani ukoloni mambo leo unaofanywa na Ufaransa katika nchi za Afrika hususan makoloni ya zamani ya nchi hiyo.
Baadhi ya waandamanaji hao wameitaka Ufaransa na wakoloni wa zamani kuilipa fidia Afrika kutokana na kupora utajiri na maliasili za bara hilo na maafa yaliyofanywa na wakoloni hao katika nchi za bara hilo. Maandamano hayo yametayarishwa na jumuiya 80 za Kifaransa na Kiafrika na kuhudhuriwa na vyama vya upinzani.
*****************************
Rais Obama azungumzia milipuko ya mabomu Uganda
Watu 76 waliuawa Uganda, baada ya kutokea milipuko ya miwili ya 
mabomu Watu 76 waliuawa Uganda, baada ya kutokea milipuko ya miwili ya mabomu
 Rais Barack Obama wa Marekani akizungumzia milipuko miwili iliyotokea nchini Uganda, amesema makundi kama Al-Shabab na Al-Qaeda hayathamini maisha ya Waafrika na kwamba wanalenga bara la Afrika kuwa eneo la kuwaua watu wasio na hatia. Katika mahojiano na Shirika la habari la Afrika Kusini, Obama ambaye ana asili ya Kiafrika alisema matamshi wanayotoa makundi hayo yenye itikadi kali, yanaonyesha wazi maisha ya watu wa Afrika hayana thamani. Rais huyo wa Marekani aliongeza kuwa Al-Shabab na Al-Qaeda sasa wanalichukulia bara la Afrika kama jukwaa muafaka la kutekeleza itikadi zao kali, pamoja na kuwauawa watu wasio na hatia bila ya kujali athari za muda mrefu.
***************************
Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi juu ya hatua ya Israel ya kubomoa nyumba za Wapalestina 
 Sample ImageMwakilishi wa Umoja wa Mataifa Mashariki ya Kati Robert Serry ameelezea wasiwasi wa taasisi hiyo ya kimataifa kuhusu hatua ya askari wa utawala ghasibu wa Israel ya kuendelea kuharibu nyumba na makazi ya wananchi wa Palestina katika eneo la Quds Mashariki. Serry ameyataka makundi yote ya Palestina na Israel kutochukua hatua yoyote ya kichochezi.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uamuzi wa Israel wa kujenga vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Ukingo wa Magharibi ni kinyume na sheria za kimataifa.
Jumanne ya jana askari wa utawala ghasibu wa Israel walivamia nyumba kadhaa za Wapalestina katika eneo la Quds Mashariki na kuziharibu kabisa. Hatua hiyo imelaani na mashirika na jumuiya mbalimbali za kimataifa za kutetea haki za binadamu. Jumuiya hiyo zimeutaka Umoja wa Mataifa kukomesha vitendo vya kibaguzi vya utawala ghaibu wa Israel huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

0 comments:

Post a Comment