Mahakama yaamuru Lubanga kuachiwa huru
Thomas
Lubanga
Majaji katika mahakama ya
kimataifa ya uhalifu huko the Hague imemwamuru mshukiwa katika kesi ya
kwanza-Thomas Lubanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-aachiliwe
huru.
Hata hivyo, hatoachiwa huru kwa takriban siku
tano, huku waendesha mashtaka wakifikiria iwapo wakate rufaa au la.
Kesi hiyo iliahirishwa wiki iliyopita baada ya
majaji kugundua kuwa kuna taratibu zilizokuwa hazijafuatwa.
Bw Lubanga amekana mashtaka ya kuwatumia watoto
kama wanajeshi.
Ofisi ya mwendesha mashitaka- Luis Moreno
Ocampo- imeonekana kutoweza kumpata shahidi.
Jaji Adrian Fulford amesema Bw Lubanga anatakiwa
'kuachiwa bila masharti yeyote' akisema kuwekwa kwake kizuizini
"haikuwa kwa haki" baada ya kesi hiyo kuahirishwa.
Katika uamuzi wao, majaji wamesema: " Mshtakiwa
hawezi kushikiliwa kwa misingi ya kushuku, ambapo katika hatua nyingine
hapo baadae kesi hiyo inaweza kuanza upya."
Hata hivyo, upande wa mashtaka una siku tano
kuomba rufaa, iwapo itakubalika, Bw Lubanga atabaki kizuizini mpaka
rufaa hiyo isikilizwe.
Inaaminika kuwa upnade wa mashtaka utakata
rufaa.
Kesi ya Bw Lubanga, iliyoanza mwaka 2009 baada
ya kuchelewa kwa miezi saba juu ya mgogoro wa kutumia ushahidi wa siri,
umejikuta katika changamoto nyingi za kisheria.
Shahidi wa kwanza alikanusha maelezo yake ambapo
awali alisema aliajiriwa na wapiganaji wa Bw Lubanga akirejea nyumbani
wakati akitoka shule.
Tatizo moja linaloikabili mahakama hiyo ni
kwamba Bunia- mji mkuu wa Ituri ambapo Bw Lubanga alikuwa kiongozi wa
waasi- bado inachukuliwa kama eneo la vita.
Hii inamaanisha usalama wa mashahidi hauna
uhakika.
Bw Lubanga alikiongoza chama cha Union of
Congolese Patriots (UPC), wanamgambo wa kabila ya Hema, moja miongoni
mwa makundi sita yaliyopigana kudhibiti eneo lenye utajiri wa dhahabu
kwenye mji wa Ituri kuanzia mwaka 1999 hadi 2003.
Mapigano hayo yaligeuka na kuwa vita vya
kikabila ambapo takriban watu 50,000 waliuawa na maelfu walibaki bila
makazi.
****************************
****************************
Zaidi ya watu 30 wafariki dunia kutokana na mafuriko nchini Sudan |
Watu wasiopungua 33 wamefariki dunia huku wengine wengi wakiwa hawajulikani waliko kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali zinazoendelea kunyesha mashariki mwa Sudan. Mkuu wa polisi katika wilaya ya Agige Bw. Ali Sukar amesema kuwa mamia ya mifugo pia imeangamia kwenye mafuriko hayo. Imeripotiwa kuwa mvua kali zimekuwa zikinyesha kwa siku 10 mtawalia usiku na mchana katika eneo la mashariki mwa Sudan jambo lililosababisha kutokea mafuriko hayo. Duru za polisi pia zimesema kuwa uharibifu mkubwa umesababishwa na mafuriko hayo. |
0 comments:
Post a Comment