Kocha mpya kijana kumsaidia Capello
Meneja
wa timu ya England, Fabio Capello, amekubali kuteua kocha kijana ambaye
ni mzawa wa England ajumuike na Stuart Pearce kwenye kikosi chake cha
ufundi, BBC Sport imefahamishwa.
Mkurugenzi
wa maendeleo wa chama cha soka cha England, Sir Trevor Brooking,
amesema atasaidia kuteua kocha huyo na kuwasilisha mapendekezo yake
ifikapo mwezi Disemba.
Pearce, ambaye pia
ndiye kocha wa timu ya England ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka
21, tayari yumo katika kikosi cha makocha cha Capello.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya bodi ya FA kukutana kujadili ufanisi mbovu wa timu ya England kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.
Nafasi kwa vijana
Mwandishi
wa maswala ya michezo wa BBC, Dan Roan alisema: "FA inataka Brooking na
Capello kutafuta kocha mwingine kijana kusaidia katika kikosi cha
ufundi cha timu ya taifa ya England, bega kwa bega na Stuart Pearce.
Wawili
hao watawasilisha mapendekezo yao kuhusiana na mpango wa kuendeleza
wachezaji wa kimataifa na mafunzo ya makocha, huku chama cha soka, FA,
kikiwa na shauriku ya kujifunza kutokana na England iliyokuwa
ikimwagiwa sifa, kushinda mechi moja tu.
Capello,
ambaye aliendelea na kazi yake baada ya mashindano, alisema ataelekeza
zaidi nguvu zake kuendeleza wachezaji vijana. Hatua za kwanza zitaanza
kuonekana wakati England itakapocheza na Hungaru katika mechi ya
kirafiki kwenye uwanja wa Wembley, tarehe 11 Agosti.
0 comments:
Post a Comment