Clinton, Hague wajadili suala la Lockerbie
Waziri
wa mambo ya kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, amezungumza na Waziri
wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague, kuhusu hatua ya kuachiliwa
mapema mwaka jana kwa mtu aliyepatikana na hatia ya kulipua ndege ya
Marekani mjini Lockerbie, Abdelbaset al-Megrahi.
Katika mazungumzo ya simu, mawaziri hao wawili walikubaliana kuwa uamuzi wa kuachiliwa kwa al-Megrahi kutoka jela ya Scotland na kumpeleka Libya ulikuwa ni makosa.
Bi Clinton alisema
Uingereza huenda ikatoa maelezo ya moja kwa moja katika baraza la
Congress kuhusu kuachiliwa huru kwa Bw Megrahi.
Uamuzi wa kumwachia huru al-Megrahi ulichukuliwa kutokana na sababu za kiafya na serikali ya Scotland.
Baraza
la senate la Marekani mwezi huu litajadili suala hilo, kufuatia tuhuma
kuwa shirika la BP la nchini Uingereza lilichangia katika uamuzi huo
ili liweze kupatiwa kandarasi kubwa nchini Libya.
Lakini BP, serikali za Uingereza na Libya zinakanusha madai hayo.
Al-Megrahi
aliachiliwa huru mwezi August mwaka uliopita na Waziri wa Sheria wa
Scotland kwa sababu alikuwa akisumbuliwa na saratani, na wakati huo
ilisemekana hatoweza kuishi zaidi ya miezi mitatu.
Marekani inasema kuna masuali ambayo yanapaswa kujibiwa kuhusu maelezo ya afya yaliyosababisha kuachiliwa huru kwa Bw Megrahi.
Alihukumiwa
kifungo cha maisha mwaka wa 2001 kutokana na kulipuliwa kwa ndege mjini
Lockerbie, ambayo iliwauwa watu 270 wengi wao wakiwa raia wa Marekani.
Karibu
mwaka moja sasa anaendelea kuishi, hali ambayo ilizusha hasira miongoni
mwa makundi yanayowatetea waathiriwa wa mkasa huo.
0 comments:
Post a Comment