SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 15, 2010

JK apokea 10ml kutoka TAG kwa ajili ya Mashuka hospitali ya Dodoma,Afungua Mkutano Mkuu wa TAG
Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Dr.Barnabas Mtokambali akimkabidhi JK hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni kumi(10m/) kama mchango wa kanisa hilo kwa ajili ya kununulia mashuka ya wagonjwa kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano Mkuu wa Kanisa hilo uliofanyika chuo Kikuu Dodoma ambapo JK alikuwa mgeni rasmi,JK alikabidhi mchango huo kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhandisi Dr.James Nsekela.
akiwa ameshika bendera ya taifa pamoja na Maaskofu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God wakati wa sala maalumu ya kuiombea amani na ustawi Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa kanisa hilo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana.Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo.
akiwahutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God katika ukumbi wa Chimwaga chuo Kikuu cha Dodoma leo mchana
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God wakionyoosha mikono wakati wa sala maalumu ya kuiombea amani na ustawi Tanzania wakati wa mkutano mkuu wa kanisa hilo uliofanyika katika chuo kikuu cha Dodoma leo mchana.
(picha na Freddy Maro)
*********************************
Dr. shein na dr. bilal wawasili zanzibar leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein na Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakiwapungia mikono wananchi mbalimbali wa mji wa Zanzibar walipowasili katika bandari ya Malindi Zanzibar leo mchana.
(picha na Amour Nassor VPO)

0 comments:

Post a Comment