Campbell aamrishwa kuwepo kesi ya Taylor
Mahakama ya kivita ya Sierra
Leone imemuamrisha mwanamitindo mashuhuri wa kimataifa Naomi Campbell
akatoe ushahidi katika kesi dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia , Charles
Taylor.
Inadaiwa mwanadada huyo alipokea pandikizi la
almasi kutoka kwa Bw Taylor kama zawadi kwake miaka 13 iliyopita.
Waendesha mashataka wanadai Campbell alitunukiwa
"almasi ya damu" mnamo mwaka 1997 nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Afrika
ya Kusini Nelson Mandela.
Bwana Taylor anashutumiwa kutumia almasi kama
hizo kuchochea vita nchini Sierra Leone.
Bi Campbell ambae ni raia wa Uingereza
alikwishawahi kukataa kutoa ushahidi wowote kuhusu kesi hio lakini sasa
ameamrishwa afike katika mahakama hiyo mjini the Hague Julai 29.
Mnamo mwezi wa Aprili aliondoka kwa hasira
kutoka kituo kimoja cha televisheni wakati alipoulizwa kuhusu uhusiano
wake na Charles Taylor -- akiangusha kamera ya kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment