Ajali ya boti Congo 'yaua 140'
Boti moja iliyokuwa imebeba abiria na bidhaa imepinduka kwenye mto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kusababisha vifo vya takriban watu 140.
Ajali hiyo imetokea katika mto wa Kasai- vijito vya mto Congo- katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo.Polisi wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa boti hiyo ilikuwa imejaa kupita kiasi.Baada ya miongo kadhaa ya migogoro, Kongo ina barabara chache au reli, inayosababisha wengi kusafiri kwenye boti hizo zilizojaa pumoni.Mwezi Novemba iliyopita takriban watu 73 walifariki dunia baada ya boti kuzama kwenye ziwa, pia katika jimbo la Bandundu.Ajali iliyotokea hivi karibuni ilitokea siku ya Jumatano.Boti hiyo ilikuwa ikibeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu, mji mkuu katika jimbo hilo.Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo ameliambia shirika la habari la Reuters, " Boti hiyo ilijaa pumoni na haikuweza kuhimili kupita kwenye dhoruba hiyo."
0 comments:
Post a Comment