SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 29, 2010


Dk Asha Rose Migiro Amtembela Rais Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rozi Migiro leo asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete Akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rozi Migiro mara tu Baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es salaam na Kufanya naye Mazungumzo Leo asubuhi.Picha na Ikulu



Rais Jakaya Kikwete Amteua Balozi Francis Malambugi Kuwa Balozi Wetu Mpya Nchini Brazil
Balozi Francis Malambugi
--
Na Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi kuwa Balozi wa Tanzania Brasilia nchini Brazil .
Uteuzi wa Balozi Malambugi umefuatia kutokana na aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika.
Balozi Malambugi ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria na Mwanadiplomasia alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 1/1/1978 kama Wakili wa Serikali na amewahi kufanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Angola, Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Geneva, Ujerumani,Ethiopia na Ubelgiji.

0 comments:

Post a Comment