Wanachama Wa CCM Morogoro Wajitokeza Kwa Wingi
Kumdhamini Rais Kikwete
Mmoja wa Wanachama wa CCM Tawi la Mkambarani , Wilaya ya
Morogoro , akiwa wamejitokeza kuweka udhamini wa fomu ya kuomba
kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM ya Rais Jakaya
Kikwete
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Wilaya ya Morogoro vijijini kichama, Mohamed Mzee (kushoto) akiwa miongoni mwa wana CCM 16 waliojitokeza kudhamini fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho. Mjumbe wa Kamati Maalum, Mariam Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ( kushoto)akiikagua kadi ya CCM ya Mwanachama , Mzee Athuman Mohamed Dume ( kulia) wa CCM Tawi la Fulwe, Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro kabla ya kukubaliwa kudhamini fomu ya mgombea wa kuomba kuteuliwa na CCM katika nafasi ya Urais wa Tanzania kwa miaka mitano , Rais Jakaya Kiwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, zoezi hilo lilifanyika Juni 22, mwaka huu.

Mzee Sudi Sarah YanyeYange ambaye ni mwanachama wa CCM
Tawi la Fulwe, Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro akiweka saini yake
katika fomu ya udhamini wa mgombea wa kuomba kuteuliwa na CCM kuogombea
nafasi ya Urais wa Tanzania kwa miaka mitano , Rais Jakaya Kiwete ambaye
ni Mwenyekiti wa CCM Taifa , baada ya kujaziwa maelezo na Mjumbe wa
Kamati Maalum, Mariam Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ( kushoto) zoezi hilo
lilifanyika Juni 22, mwaka huu.
Juu na chini ni baadhi ya Wanachama wa CCM Tawi la
Mkambarani , Wilaya ya Morogoro , wakiwa wamejitokeza kuweka udhamini wa
fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM ya
Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho,
zoezi hilo lilifanyika Juni 22, mwaka huu.
********************************
Na John Nditi,
Morogoro
WANACHAMA 378 wa chama cha Mapinduzi ( CCM) kutoka Wilaya ya Morogoro wamejitokeza kumdhamini, fomu ya mgombea wa kuomba kuteuliwa na CCM katika nafasi ya Urais wa Tanzania kwa miaka mitano , Rais Jakaya Kiwete .
Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, amechukua fomui kwa ajili ya kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Rais Kikwete alichukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo kubwa Juni 21, mwaka huu Makao Makuu ya Chama hicho Mjini Dodoma.
Wanachama wa chama hicho waliomdhamini ni kutoka Manispaa ya Morogoro na Morogoro Vijijini , ambapo kwa Manispaa Mwanachama wa kwanza kuwekea udhamini wake aliyewahi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro , Kanali Mstaafu Izack Mwisongo.
Mbali na Mwenyekiti Mstaafu huyo wa CCM Mkoa wa Morogoro, mwingine alikuwa ni Katibu wa CCM Mstaafu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, ambaye pia ni Kapteni mstaafu, Nicholaus Mvanga.
Baadhi ya viongozi wengine wa ngazi za chama hicho waliojitokeza kudhamini fomu za Mgombea wa Urais kupitia CCM, ni Katibu wa CCM Tawi la Mbete, Kata ya Mlimani, Asha Almasi pamoja na Mwenyekiti wa UWT Kata ya Sultan Area, Anuni Jafari.
Kwa upande wa Morogoro vijijini , mgombea huo alipata wadhamini 46 kutoka Matawi ya Mkambarani, Fulwe na Gwata Ujembe, katika Tarafa ya Mikese ambao wengi wao walikuwa ni wazee , vijana na akina mama.
Katibu wa Kamati ya Kusajili wadhamini Kanda ya Mashariki yenye kujumiisha Mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam, Alexandaer Nchimbi alisema wanaccm wenngi walijitokeza kumdhamini mgombea wao Rais Kikwete ,lakini kutokana na muda kuwa mdogo wengi wameshindwa kutimiza kusudio lao.
Nchimbi ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM), alisema baada ya kupata wadhamini wengi katika Mkoa wa Morogoro, siku hiyo waliekelea Mkoa wa Tanga na baadaye kuwenda Pwani na kumalizika Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati huyo ya Kanda ya Mashariki, idadi hiyo kubwa imaonyesha kuwa wananchi na wanaccm bado wanaimani ya uongozi wa Rais Kikwete na hivyo kujitokeza kumdhamini ili awezekuteuliwa na kuchaguliwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Ujumbe wa Kamati hiyo uliambatana na Mwenyekiti wa kitaifa wa uratibu wa zoezi la kupata wadhamini wa fomu ya mgombea huyo zilizogawanywa kuwa Kanda sita na kuhudhuiria katika zoezi lililifanyika Ofisi ya CCM Mkoa wa Morogoro.
Katibu Msaidizi Mkuu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Eliud Shemauya, alisema zoezi hilo lilifanyika katika Wilaya mbili za kichama ya Mororogoro mjini na Vijijini ambapo wanachama wengi walijitokeza.
Alisema kwa upande wa Morogoro vijijini , wanachama wa Matawi ya Mkambarani , Fulwe na Gwata Ujembe walijitokeza licha ya kupewa taarifa ya muda mfupi na kwamba hakukuwa na uwezekano wa kusambaza fomu hizo kwenye wilaya nyingine kutoka na muda kuwa mdogo.
Nao baadhi ya wanachama waliopataa fursa ya kumdhamini Mgombea wa CCM , Rais Kikwete, walisema kuwa wamejitokeza kwa wingi kutokana na kutanmbua mchango aliouleta katika uongozi wake wa kipindi cha miaka mitano hadi 2010.
Mzee Sudi YanyeYange, ni kati ya mwanachama aliyepata fursa ya kumdhamini , Rais Kikwete, alisema wazee , vijana na akina mama wamejitokeza kwa wingi kutokana na usimamizi wake bora wa ilani ya CCM ya mwaka 2005-2010.
“ mimi nimejitokeza kumdhamini kwa kuvutiwa na utendaji wake hasa kuwa mkweli , kusimamia utekelezaji wa ahadi zake anazoziahidi …zikiwemo na zile zilizoachwa na Serikali ya awamu iliyopita” alisema Mwanachama huyo
Naye Mwanachama Asha Almas ambaye ni Katibu wa CCM Tawi la Mbete, Kata ya Mlimani , Manispaa ya Morogoro, alisema ameamua kumwekea udhamini kwenye fomu yake kutokana na utendaji bora wakiwa madarakani na kabla ya kuwa madarakani mwaka 2005.

0 comments:
Post a Comment