MADAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA KINAMAMA
DUNIANI WAKUTANA DAR LEO!!!!!!
Aidha Mama Salma amesema vifo vya wazazi na hapa nchini Tanzania
bado ni vya kusikitisha mno kwani kiwango cha vifo vinavyo sababishwa na
uzazi hukadiriwa kufikia kiwango cha wanawake 578 kwa kila vizazi hai
100,000
Akihitimisha Mama Salma kikwete amesema Uboreshaji wa uwigo wa
huduma ni muhimu katika kufikia lengo la maendeleo la Milenia la 4,5na
6,lililoridhiwa na Tanzania katika kupunguza vifo vya akina mama kwa
robo Tatu kutoka 578 hadi 193 kwa vizazi hai 100,000, na vifo vya watoto
wachanga kutoka 32 hadi 19 kwa vizazi hai 1,000.
Pamoja na kuwa warsha kama hizi hufanyika kila mara kwa mara
lakini Je walengwa wa mahitaji hayo hufikiwa kwa mda mwafaka?kauli mbiu
ya warsha hiyo ni‘CHANGAMOTO KATIKA AFYA YA WANAWAKE:USHAHIDI WA
KIUTENDAJI”amesema Mama Salma na ni matumaini yake kuwa FIGO na AGOTA
wataongeza ushirikiano katika kuisaidia Tanzania kupunguza tatizo la
vifo kwa wazazi na watoto.
Pichani ni Upande wa Kushoto wa Ukumbi wakiwa wamekaa
Pichani ni Upande wa Kushoto wa Ukumbi wakiwa wamekaa
madaktari bingwa wa Magonjwa ya Kina mama
kutoka sehemu
mbalimbali duniani wakisiliza kwa makini hotuba ya Mgeni
rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa Uzinduzi wa Warsha hiyo.
0 comments:
Post a Comment