Ujerumani leo kumpata rais mpya
Mgombea urais wa Ujerumani kwa tiketi ya CDU/FDP Christian Wulff
Rais mpya wa Ujerumani
anachaguliwa , leo na baraza maalumu la shirikisho lenye wajumbe
1244.
Atakaechaguliwa leo atachukua nafasi ya rais wa hapo awali, Horst
Köhler, aliejiuzulu mwezi uliopita.
Wanagombea wadhifa huo ni waziri mkuu wa sasa wa jimbo la Lower
Saxony, Chrsitian Wullf, na aliekuwa anasimamia idara kuu ya
nyaraka za siri za idara ya ujasusi wa ndani ya Ujerumani
Masharrikiya hapo awali, Bwana Joachim Gauck, mwenye umri wa miaka 70.
Waziri Mkuu Christiana Wullf ni mjumbe wa vyama vya serikali ya
mseto na CDU na chama cha Waliberali, FDP. Vyama hivyo kwa pamoja
na chama ndugu cha CSU vitawapeleka wajaumbe 644 yaani 21 zaidi
ya wingi unaohitajika ili mjumbe wao ashinde .
Mgombea mwingine, Joachim Gauck, ni mgombea anaeungwa mkono na
vyama vya upinzani-SDP na chama cha kijani. Kwa pamoja vyama hivyo
vitawapeleka wajumbe 462.
Lakini Gauck mwenyewe hayumo katika chama chochote .
Kwa hiyo, hesabu zinaonyesha kwamba mgombea wa vyama vya serikali
anatarajiwa kupita katika kinyang'anyiro cha leo.
Wagombe hao ni watu wanaotofautiana kwa namna nyingi .
Kwanza kabisa mgombea wa vyama vinavyoongoza serikali,
Christian Wullf, amekulia katika upande wa Magharibi wa Ujerumani.
Mgombea wa vyama vya upinzani, Joachim Gauck, alikuwa mwanaharakati
wa kupigania uhuru katika sehemu ambayo hapo zamani ilikuwa
inaitwa Ujerumani ya mashariki.
Juu ya hayo mgombea huyo amesema:
Joachim Gauck,
"Tulikuwa Mashariki kwa sababu
tulilazimishwa .Lakini katika fikira zetu tulikuwa na wazo la uhuru
ambao haukuwapo katika upande wa Mashariki, lakini ulistawi katika
Magharibi."
Joachim Gauck, asiyekuwa na chama chochote, hana matatizo na
wahafidhina na Waliberali. Kwani angeliweza kuwa mgombea wa vyama
vya serikali na vyama vya upinzani kadhalika.
Vyama vya upinzani vilimpendekeza Gauck. Kansela wa Ujerumani
alipewa taarifa lakini alilikataa pendekezo hilo japo anamthamini
sana Bwana Gauck.
Mgombe mwingine Christian Wullf aliependekezwa na vyama
vinavyoingoza serikali . Christian Wullf alianza kuvuta pumzi ya
uhuru tokea siku ya kwanza alipozaliwa katika Ujerumani magharibi.
Wullf mwenyewe anasema.
´´Muhimu ni kwamba natoka katika nasaba ya kati na nadhamiria
kubakia katika nasaba hiyo. Kwangu ni jambo la kuvutia ikiwa rais
atakaefuatia atakuwa mtu anaetoka katika rika la kati. Mtu mwenye
uzoefu wa kuleta pamoja kazi na majukumu ya familia´´.
Christiana Wullf ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa leo kuwa rais
mpya wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani.
Amesema akichaguliwa ataendeleza sera za Horst Köhler, rais
wa hapo awali alieliweka bara la afrika moyoni.
Köhler alizetembelea nchi kadhaa za Afrika kuhudhuria vikao na
ushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mwanasiasaa huyo amesema kwake ni wazi kabisa kwamba Ujerumani
inapaswa kuuendeleza uhusiano na Afrika ulioanzishwa na rais wa
hapo awali-
Mwandishi/ Martin Beutler/ZAR/
0 comments:
Post a Comment