SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 30, 2010

Paraguay yaishinda Japan kwa penalti
Paraguay dhidi ya Japan
Paraguay iliishinda Japan kwa penalti tano kwa tatu
Paraguay imeshinda pambano la kwanza kwa mikwaju ya penalti katika michuano ya Kombe la Dunia ya 2010 na kufaulu kuingia robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake ambapo watacheza na mshindi kati ya Hispania na Ureno.
Paraguay ilifunga mikwaju yake yote mitano baada ya pambano lake na Japan kumalizika bila ya kufungana mwishoni mwa muda wa ziada.
Pambano hilo lilikosa msisimko wakati kila upande ukijidhatiti kulinda lango lao.
Matumaini ya Japan yalitoweka baada ya Yuichi Komano kugonga mwamba.
Paraguay iliibuka na ushindi wa penalti tano kwa tatu.
Kushindwa kwa Japan kulimaanisha bara la Asia halitakuwa na mwakilishi katika duru ya robo fainali.
*********************************
Uhispania yaingia robofainali
 
David Villa akishangilia bao aliloifungia Uhispania dhidi ya Ureno David Villa akishangilia bao aliloifungia Uhispania dhidi ya Ureno
Mabingwa Ulaya Uhispania imekuwa nchi ya mwisho kufuzu kwa robofainali ya michuano hiyo ya kombe la dunia baada ya kuichapa Ureno bao 1-0 katika mechi iliyokuwa kali na ngumu.
Alikuwa ni mshambuliaji hatari wa timu hiyo David Villa aliyewarejesha nyumbani Ronaldo na wenzake, kwa bao la dakika ya 63 na kufufua matumaini kwa Uhispania kuweza kutwaa ubingwa huo.Uhispania ni miongoni mwa timu ambazo zinapigiwa sana upatu kushinda taji hilo, hata mfalme wa kandanda duniani Pele ni miongoni mwa wale wanapiga upatu huo.
Timu nyingine zilizofuzu kwa robofainali ni pamoja na  Paraguay, Ujerumani, Ghana, Brazil, Argentina, Uholanzi na Uruguay.
Paruguay ilifanikiwa kuingia hatua hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya kabumbu la nchi hiyo baada ya kuitoa Japan kwa changamoto ya mikwaju ya penalti, kufuatia kila mtu kutoweza kuufumania mlango wa mwenzie hata pale mpambano uliporefushwa muda.
Mshambuliaji nyota wa timu hiyo Santa Cruz alisema kuwa kufuzu kwa hatua hiyo, ni ndoto aliyokuwa akiiota na kwamba sasa imekuwa kweli.Amesema kwa kipindi cha miaka minne iliyopita wamekuwa wakiota fainali za mwaka huu kufanya vyema.
Mechi mbili za kwanza za  robofainali zitakuwa Ijumaa ijayo kwa pambano kati ya Brazil na Uholanzi na baadaye Ghana na Uruguay. Jumamosi itakuwa zamu ya Ujerumani kuumana na Argentina na hatimaye Uhispania kucheza na Paraguay.

0 comments:

Post a Comment